Mwongozo wa Bwana Chui wa Muziki wa Kiafrika       
Mwanzo    Wanamuziki, tafuta    Makala na mahojiano    Viungo   
Franco

HISTORIA YAKE
MAKALA

SAHANI:
FRANCO, JOSKY,
 MATALANZA

THE VERY BEST OF
ROUGH GUIDE TO
 FRANCO

    

 


1938-1989
CONGO, JAMHURI YA DEMOKRATIA

Homepage, unofficial

Ama:
Francois Luambo Makiadi

Memba wa:
TPOK Jazz

Lugha:
Kilingala

Mtindo:
Soukous
Rumba congolais

Ala:
Gitaa
Waimbaji wa kiume

Makala:
Retroafric
Afropop
Introduction to Franco
Remembering Franco

Kwenye mtandao
Sahani
Rumba congolais/music samples
Franco songs

Biography


Ingawa ni Joseph Kabasele Aka "Le Grande Kalle" aliyeanzisha mtindo wa muziki wa kisasa wa kikongo, ni Franco ndiye baba wa taifa ki muziki, au tuseme wa Afrika nzima. Ujuzi, ujasiri na utaalamu wake wa kupiga gitaa, uliweza kuweka kiwango cha kawaida (standard) cha jinsi ya kupiga gita- hakujatokea mabadiliko yeyote hadi sasa ingawa ni karibu miaka 11 tangu afariki. Ingawa kwa cheo yeye alikuwa wa tatu katika bendi maarufu ya OK Jazz, yeye ndiye alikuwa kiongozi bila kupingwa. Sababu zilikuwa nyingi. Alikuwa na tabasamu la ujana, na daraja la juu kama "nyota". Katika maisha yake ya kimuziki, alikuwa na kipaji alichopewa na Mungu cha upigaji gitaa, lakini kwanza kabisa: Aliimba juu ya mambo ya kawaida yaliyowahusu watu, na historia ya matukio ya kila siku ya watu katika mitaa ya jiji la Kinshasa, na kuandikwa kwa lugha ambayo watu waliielewa, kwa sababu ilitokana na matukio ya kila siku ya mitaani. Franco pia aliimba juu ya maswala makubwa, juu ya uadilifu, juu ya kuwa muafrika, juu ya ukimwi ("Attention Na SIDA" ya mwaka 1987 ni na imekuwa klassiki ya kiafrika), na juu ya uhusiano kati ya mwanaume na mwanamke, ambao umeandikwa mara nyingi sana katika muziki wa pop wa ulaya. Hata hivyo ni vilevile kama ilivyo. Franco alipiga muziki wa pop kwa mtindo mzuri sana wenye burdani, na wa kuliwaza na bila kusahau, muziki wa kudensi. Kwa sababu ya kujihusisha sana na mambo ya kiafrika na matukio ya kila siku yawapatayo watu, alikuwa maarufu mbele ya kadamnasi katika bara zima, na gazeti la kiingereza la "Folk Roots2 lilipomtaja Youssou N'dour kama "Mwanamuziki wa kiafrika wa karne hii", watu walishikwa na bumbuazi na kusema kuwa ni mzungu mjinga ambaye angeweza kumuweka mwanamuziki mwingine juu ya franco katika uteuzi wa namna hii. Franco alipofariki mwaka 1989, Zaire (sasa Kongo-Kinshasa), ailifanya maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku 4, na studio za ardio zilitoa muziki mfululizo wa kudensi ambao haujawahi kutolewa hata siku moja. Hatusemi zaidi.
Rekodi za Franco zimekuwa adimu sana kupatikana nchini norway, pamoja na kuwa zimetolewa kwa wingi sana: yapata kama albamu 150 zimetolewa, lakini baadhi ya rekodi zake za zamani zinapatikana kwenye mkusanyo wa "Roots of OK Jazz" na "Azda" ambayo ipo kwenye kampuni ya rekodi ya kifaransa ya Sonodisc.
(Lakini kuna dalili za kurudiwa uvumbuzi na utoaji wa rekodi mpya mara kwa mara)

Arne Berg

Wanamuziki wanaohusiana:
Papa Noel
Sam Mangwana
Papa Wemba

 A   B   C   D 
 E   F   G   H 
 I    J   K   L 
 M   N   O   P 
 Q   R   S   T 
 U   V   W   X 
 Y   Z 
COMPILATIONS
WANAMUZIKI A-Z

KJØP PLATE

 

Tadhibiri mpya:
22 nov 2009

  
Rudi juu



    

FRANCO, JOSKY, MATALANZA  
Sonodisc/1994

Wapiga gitaa watatu, waimbaji watatu. Hawa vijana wanakiweza kile wanachokifanya. Magitaa yanapangilia mapigo juu ya mapigo, na kwenye shina kuna mapigo ya kiafrika ya ngoma na marakasi. Wimbo unaendelea na kuendelea tu. Rekodi inaanza na wimbo mrefu wa dakika 13 wa "Partagez" ambao unachukua hatua toka mwanzo, Franco anaimba sauti ya kwanza, Josky na Matulanza wanajibu na kuukimbiza wimbo katika hali ya kasi kabla Franco hajapokea na gitaa lake baada ya dakika 5. Looh! Halafu vijana wanaingia kwa magitaa ya solo namba mbili-!
Hivi ndivyo wanavyoonyesha ufundi wao wa kushawishi katika rekodi yote, wanafikia kiwango cha juu katika wimbo wa "Laissez-passer" (ambao pia unapatikana kwenye "Very best of").
Pengine inakuwa ni wimbo uliotiwa chumvi nyingi na kuchezea magitaa, imekuwa ni vurugu tu kwa mzaliwa wa Ulaya ya kaskazini ambaye hakujitayarisha. Muziki wa kiafrika umeundwa katika mtindo wa kujirudiarudia mara nyingi. Lakini hiyo ni safi tu.

 

KJØP PLATE
Rudi juu



    

THE VERY BEST OF  
Manteca/2000

Afadhali!
Hapa tuna rumba kabambe ya kuokea kile tulichojaribu kutafuta kwa miaka mingi kufikia chaguo la rekodi za Franco bila kufanikiwa. Mara inatuijia kampuni mpya ya rekodi ya kiingereza ya Manteca na albamu mpya kabambe! Siwezi kusema kuwa nazifahamu vizuri rekodi zote za Franco, kiasi cha kuelezea juu ya zote zilizorekodiwa hapa kwamba ndizo nzuri kati ya zote- ni kazi ngumu. Hata hivyo, Manteca ameweza. Hapa wanatoa nyimbo za klassiki, nyingine baada ya nyingine. Unaanza wimbo wa OK Jazz ujulikanao ambao kwa watu wa Norway unasikika kama: Umekuja OK, ondoka KO. Halafu inaendelea kwa wimbo hadi wimbo. Nyimbo za Franco zimegawanyika katika sehemu mbili, magitaa yenye mapigo ya jazz, kabla hajaingia kwa nguvu karibu na mwishoni na rumba ya nguvu kama katika wimbo wa "Azda" au "Attention. Na SIDA". Albamu hii ni historia ya ki muziki, unaisikiliza na kujisikia kwa muda wa miaka mingi katika vibao vya muziki wa kiafrika vya mwanamuziki maarufu sana wa Afrika katika karne iliyopita. Na muziki wake bado uko hai kabisa.

 

KJØP PLATE
Rudi juu



ROUGH GUIDE TO FRANCO
World Music Network/2001

KJØP PLATE
Muhariri: Bjørn-Erik Hanssen
post(a)leopardmannen.no

Mwanzo    Wanamuziki, tafuta    Makala na mahojiano    Viungo   

Rembo: Idar Lind
English: Katherine Stewart-Kreisman
Swahili: Francis Chagula (francis.chagula@malvik.kommune.no)
Swahili: Habiba Rajabu (habiba@online.no)
Bendera: 3Dflags.com

This site is a member of WebRing. To browse visit here.

Another possibility.

Go deeper.