Mwongozo wa Bwana Chui wa Muziki wa Kiafrika       
Mwanzo    Wanamuziki, tafuta    Makala na mahojiano    Viungo   
Tranzania, Acid Queen

HISTORIA YAKE

SAHANI:
TRANZANIA

    

 

TANZANIA

Ama:
Stephan Groth
Christian Grimshei

Mwanamuziki wa:
Sisi kwa Sisi
Egyptian Musical Club

Lugha:
Kiswahili

Mtindo:
Taarab
Techno

Ala:
Syntesizer
Fidla
Ngoma
Waimbaji

Historia yake

Shirika la kutoka Norway linaloitwa “Kirkelig Kulturverksted” limefanya jaribio la kishujaa! Pamoja na shirika la umeme la Norway, kampuni ya radio ya Norway (Norwegian Radio Programme 2) na NORAD, wametoa CD inayoitwa TRANZANIA. Toleo hili ni la ushirikiano kati ya kundi la kinorwegian linaloitwa “Acid Queen” (wahusika wa bendi hii ni Stephan Groth na Christian Grimshei), pamoja na makundi mengine mawili yanayotoka Dar es Salaam, kundi la Sisi Kwa Sisi na kundi la Egyptian Musical Club. matokeo ya ushirikiano wa makundi haya ni kwamba, wamepiga muziki wa aina ya taarab kwa kisasa. Utengenezaji wa hii CD ni sehemu ndogo tu ya mradi ambao lengo lake ni kutetea na kuleta usawa kwa wanamuziki wa kitanzania, chini ya shirika linaloitwa CHAMUDATA.

Wanamuziki wanaohusiana:
Zuhura Swaleh

 A   B   C   D 
 E   F   G   H 
 I    J   K   L 
 M   N   O   P 
 Q   R   S   T 
 U   V   W   X 
 Y   Z 
COMPILATIONS
WANAMUZIKI A-Z

KJØP PLATE

 

Tadhibiri mpya:
22 nov 2009

  
Rudi juu



    

TRANZANIA  
Kirkelig Kulturverksted/1999

Upende usipende unajikuta umenogewa sana wakati wanamuziki wa bendi ya kinorwegian ya Acid Queen wakichanganya vizuri wanapopiga taarabu. Hii ni kweli ingawaje hii CD ilitayarishwa sana sana kwa ajili la soko la ulaya.
Kikundi hichi kiliiga mtindo alioufanya Jan Garabarek alipotumbuiza na Hillary Ensemble. Yaani, walijaribu kwa kubahatisha tu na wao wakachanganya utamadunu/mila mbili ambazo hazihusiani na zipo tofauti kabisa. Alivyofanya Garabarek ni kuchanganya saksafoni, ambacho ni chombo cha kisasa, pamoja na kwaya iliyokuwa inaimba nyimbo na sauti za enzi ya kale sana (mediaeval choir sounds.) Wakati akina Acid Queen walichanganya muziki wa kisasa wa ulaya aina ya “techno”pamoja na muziki wa asili wa taarabu. Kwa kweli jaribio hili lilikuwa kabambe na lenye ujuba!
Nyimbo nzuri zaidi za CD hii ni zile zilizojaribu kuchanganya mitindo hii miwili, kama kwa mfano katika wimbo wa “Sema” na “Yalaiti”. Mchanganyiko huu ulipofanikiwa kwa kweli ulipendeza sana. Katika wimbo wa kwanza wa “Sema” tunaingia katika usiku wa Afrika Mashariki ambapo unasikia sauti za nyenze/panzi pamoja na bendi ya taarab ikitumbuiza kwa nyuma. Wakati huo huo muziki wa kisasa wa vijana ukijipenyeza katika mdundo unaowiana na ule muziki wa taarab. Na wakati sauti nzito ya mwimbaji wa Egyptian Music Club inapoanza kumiminika juu ya vyote, basi kinaibuka kitu kipya na cha kusisimua ambacho kinagusa na kutia shauku vikiwa sambamba na utamaduni. Wimbo huu unaochukua zaidi kidogo ya dakika saba unapandisha madadi kama ilivyo kawaida ya muziki wa Kiafrika. Una mapigo ya mzunguko, ambayo yanarudiwa mara nyingi, yakibadilishwa kidogo tuu kwa madoido ya hapa na pale yanaoufanya mwimbo kuendelea. Kwa ujumla ni mwimbo mzuri tokea mwanzo hadi mwisho.Tunaweza kutoa muhtasari huu huu kwa wimbo wa “Yalaiti”. Hapa wanamuziki wamechanganya vyombo pamoja na kiitikio cha kundi la Sisi Kwa Sisi, ambalo ni kundi mojawapo la taarabu kati ya makundi mawili yaliyoshiriki kwenye hii CD.

KJØP PLATE
Muhariri: Bjørn-Erik Hanssen
post(a)leopardmannen.no

Mwanzo    Wanamuziki, tafuta    Makala na mahojiano    Viungo   

Rembo: Idar Lind
English: Katherine Stewart-Kreisman
Swahili: Francis Chagula (francis.chagula@malvik.kommune.no)
Swahili: Habiba Rajabu (habiba@online.no)
Bendera: 3Dflags.com

This site is a member of WebRing. To browse visit here.

Another possibility.

Go deeper.